Recent Post

Side Add

No available add

Ni timu gani inayofaa kushabikiwa na Afrika kombe la Dunia?

MUHAMMED KHATIB

Nyoyo zilivunjika baada ya mataifa yote ya Afrika kama vile Senegal, Nigeria, Egypt, Morocco na Tunisia - kung'olewa katika awamu ya kwanza ya kimakundi ya kombe la dunia-lakini licha ya hivyo matumaini ya mashabikji wengine hayajavunjika.

''Bado tuna Ufaransa'' , watu wengi wamefanya mzaha katika mitandao ya Kijamii.

ata rais wa Ufaransa Emmanuel Macron hakuwanywa nyuma alipowaambia mashabiki wa Nigeria kuishabikia Ufaransa baada ya Nigeria kuondolewa.

Ruka ujumbe wa Twitter wa @EmmanuelMacron

Emmanuel Macron?@EmmanuelMacron

As the Super Eagles are no longer in the competition, please support the French Team in the Football World Cup!

9:12 PM - Jul 4, 2018

Twitter Ads info and privacy

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @EmmanuelMacron

Ni kweli kwamba, Ufaransa ina wachezaji 14 katika kikosi hicho ambao wanaweza kulichezea taifa la Afrika.

Wachezaji wawili wa Ufaransa wana vizazi vinavyotoka bara hili. Nduguye Paul Pogba, Florentin anaichezea Guinea , huku nduguye Steve Mandanda , Parfait, akiwa anaichezea timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

Wote waliichezea timu ya taifa ya Ufaransa ya vijana kabla ya kuamua kuwakilisha mataifa ambayo wazazi wao wanatoka.

Kikosi cha kombe la dunia cha UfaransaHaki miliki ya 

Wachezaji 14 kati ya wachezaji 23 wa Ufaransa wangeweza kuliwakilisha bara la Afrika

Kinda wa Ufaransa ambaye ameibuka kuwa mchezaji bora mwenye umri mdogo katika kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 19 Kylian Mbappé, alizaliwa na baba raia wa Cameroon na mama mwenye mchanganyiko wa uraia wa Ufaransa na Algeria.

wengineko Ubelgiji , ina wachezaji wanane walio na mizizi ya bara Afrika- huku mmoja ama hata wazazi wote wawili wakitoka katika bara la Afrika.

Wachezaji hao ni Fellaini, Lukaku, Dembélé, Boyata, Batshuayi, Chadli naTielemans.


Sheria za Fifa kuhusu uraia

Shgeria za Fifa kuhusu uraiaHaki miliki ya FIFA

  • Mchezaji aliyeichezea timu moja ya taifa katika mchuano mkubwa hawezi kuhamia taifa jengine.
  • lakini sheria hii imepunguzwa makali kuwaruhusu wachezaji kubadilisha uraia kutoka timu za vijana hadi zile za taifa
  • Mechi za kirafiki hazimzui mtu- hivyobasi Diego Costa aliweza kuhamia Uhispania baada ya kuiwakilisha Brazil katika mechi za kirafiki , Mchezaji wa Ubelgiji nacer Chadli pia aliiwakilisha Morocco katika mechi ya kirafiki
  • wachezaji wasio na wazazi wanaotoka katika taifa hilo wanaruhusiwa kuwakilisha iwapo wameishi katika mataifa hayo na kuzichezea timu hizo kwa miaka mitano.
  • lakini hilo ni tofauti kwa wakimbizi , ambao wanaweza kuyawakilisha mataifa wanayoishi baada ya kupokea uraia bila ya kusubiri kwa miaka mitano.

Mchezaji anayeichezea Sweden anayehusishwa na Kenya

Pia katika michuano hiyo kuna Uingereza, Sweden , Uruguay , Brazil , Urusi na Croatia. Wachezaji walio na mizizi ya bara Afrika ni kama vile Delle Alli wa Uingereza- ambaye babake anatoka Nigeria , na mchezaji mwenza Danny Welbeck ambaye alizaliwa Manchester kutoka kwa wazazi wa Ghana.

pengine uhusiano wa Sweden na bara Afrika haujulikani sana .

John Guidetti wa Sweden aliishi nchini Kenya kwa miaka mitatu akiwa mtoto , akionyesha umahiri wake mapema kama mchezaji alipokuwa akiichezea timu ya vijana ya Nairobi Ligi Ndogo.

Mashabiki wa Kenya wamekuwa wakisambaza picha za Guidetti katika mitandao ya kijami.

Ruka ujumbe wa Twitter wa @FloSimba88

View image on Twitter

View image on Twitter

FloSimba@FloSimba88

Sweden's John Guidetti was raised in Kenya.
Who can spot him ?

11:14 PM - Jun 23, 2018

Twitter Ads info and privacy

Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @FloSimba88

"Bado nina uhusiano mzuri na Kenya na kila mara ninapokwenda nchini humo nakaribishwa vizuri sana, ," Guidetti alinukuliwa akisema katika gazeti la The Standard nchini humo.

Kocha wa zamani wa Guidetti , Chris Amimo, aliambia gazeti hilo kwamba Guidetti alikuwa akichaguliwa kila mara kuiwakilisha timu hiyo. Alipenda sana kucheza kandanda.

"Babake alikuwa akifanya kazi katika shule ya Swedish ambayo iko mkabala na uwanja wa Ligi Ndogo," aliongezea.

Huku Guidetti akishindwa kuiwakilisha Kenya kwa upungufu wa miaka miwili , mchezaji mwenza wa Sweden Martin Olsson alizaliwa na mama Mkenya hivyobasi angekuwa na chaguo la kuwakilisha taifa moja kati ya hayo maiwili

Vilevile wachezaji sita pekee kati ya 23 wa timu ya taifa ya Morocco katika Kombe la dunia ndio waliozaliwa nchini humo.

Related Posts you may like

Popular Post

Side Add

No available add